23.6 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Jumuiya ya Wazazi Taifa yapongeza Bajeti ya Tanzania Bara na Visiwani

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Jumuiya ya Wazazi Taifa imepongeza bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2024-2025, ikisema imejaa matumaini makubwa na imegusa maisha ya Watanzania kwa kuboresha huduma mbalimbali.

Jana, Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, aliwasilisha bajeti ya zaidi ya Sh trilioni 49 bungeni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023-2024 ambayo ilikuwa zaidi ya Sh trilioni 44.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Juni 14, 2024, jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Fadhil Maganya, alitoa pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, kwa kuwasilisha bajeti hiyo ambayo imeleta matumaini makubwa kwa Watanzania.

Maganya, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, alisema bajeti hiyo imejaa matumaini mema ambayo yanabeba maisha ya wananchi kwa kuboresha huduma mbalimbali.

“Mimi kama kiongozi wa Jumuiya ninampa Mheshimiwa Rais kongole. Kongole hii ni kwa kuwa bajeti hii inabeba matumaini kwa Watanzania. Kwa hiyo, tukaona kama Jumuiya tutoe kauli yetu ya kuipongeza serikali kwa namna ambavyo imeendelea kuwajali Watanzania na kuwapatia nafuu ya maisha kadri inavyowezekana,” alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha, Maganya pia alitoa pongezi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa bajeti ambayo imegusa maisha ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles