Na Mwandishi Wetu, Igunga
Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, Revocatus Kuuli.
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Kuuli leo Desemba 28, kutokana na kukabiliwa na tuhuma za kutwalia ardhi ya wananchi bila kufuata utaratibu, utendaji kazi usioridhisha na matumizi mabaya ya fedha za maduhuli ya Serikali.
“Suala laNkurugenzi wa hapa nalifahamu, nina ripoti nyingi zinazomhusi yeye na kuna wakati nilimtuma Mkuu wa Mkoa kuja kushughulikia ishu yake, sasa sababu bado hajajirekebisha ninamsimamisha kuanzia leo.
“Kuuli siyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga kuanzia sasahivi,” amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Tabora Dk. Phillemon Sengati kuteua Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo mara moja.
“Huko aliko aandikiwe barua, kwamba hana kazi ya kuwa Mkurugenzi wa hapa Igunga, kwa hiyo Mkuu wa Mkoa na uongozi wa Igunga mkae mteue mtu ambaye ananidhamu, ambaye hatadhurumu watu aanze kukaimu kabla sijapanga mipango ya kumteua Mkurugenzi mwingine wakuja hapa atakayeendana na kazi yangu,” amesema Rais Magufuli.