22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

RMO Geita apiga marufuku huduma za uzazi wa mpango bila elimu

Na Yohana Paul, Geita

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) wa Geita, Dk. Emmanuel Mkubwa amesema mkoa umejipanga kikamilifu kutoa huduma za afya ya uzazi hususani katika kitengo cha huduma ya uzazi wa mpango ambapo kila mwenye uhitaji wa huduma hiyo ni lazima kwanza apatiwe elimu kabla ya kuhudumiwa.

Dk. Mkubwa alisema hayo wiki iliyopita wakati akizungumza na gazeti hili kuelezea mwenendo wa maboresho ya huduma ya afya ya uzazi mkoani hapa na kusisitiza ofisi ya Mganga mkuu imeendelea kuwekea mkazo suala la kutoa elimu ya afya ya uzazi kabla ya kutoa huduma kamili kuwa ni la lazima.

Alisema maelekezo yaliyopo kwa watoa huduma wa afya wote mkoani hapa ni kuwa hawaruhusiwi kumuanzishia mtu yeyote dozi ya vidonge vya uzazi wa mpango bila kumpatia elimu ambapo hadi sasa maelekezo yanazingatiwa kwa kiasi kikubwa.

 Alisema wote wanaohitaji kuanza kutumia uzazi wa mpango wamekuwa wakipatiwa elimu juu ya faida na baadhi ya changamoto zinazoweza kujitokeza iwapo wataanza kutumia dawa au aina nyingine ya vidhibiti mimba na hadi sasa mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa.

Aidha, Dk. Mkubwa alitoa wito kina mamA wote kuhakikisha wanawahi kliniki mara tu wanapohisi ujauzito ili kupata vipimo vya awali na kuendelea kuhudhuria mara kwa mara ili kujua mwenendo wa mtoto tumboni pamoja na kufahamu dalili hatarishi kwa mjamzito.

Kaimu Mganga mkuu huyo aliwataka kina baba kuwahimiza wenza wao kufuata huduma za afya ambapo pia alitumia nafasi yake kuwakumbusha watumishi wote wa afya mkoani hapa kufanya kazi na kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia miongozo ya wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia na watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles