33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

JPM apiga marufuku maagizo kutoka juu

JNa MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS Dk. John Magufuli amewataka watumishi wa umma, viongozi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi na wafugaji kuongeza juhudi za uzalishaji mali katika mwaka 2019.

Pamoja na hilo pia amewataka wapige vita rushwa, wizi, ufisadi, ubadhilifu na kwamba anaamini kuwa uchumi wa Tanzania utazidi kupanda katika mwaka 2019.

Hayo aliyasema usiku wa kuamkia jana katika salamu zake za mwaka mpya 2019, ambapo aliwataka watumishi wa umma wachape kazi na wajiamini.

“Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini, waachane na utamaduni wa kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu.

“Huo ni ugonjwa ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama ni kwa mujibu wa sheria hawataki kujiamini, na wanasema hili ni maagizo kutoka juu,” alisema Rais Magufuli.

Amemalizia kwa kusema “Ninaanza kuiona Tanzania mpya inakuja, tusiiachie Tanzania mpya, tuifike, tuikae na tuiishi kwa sababu huu ndio wakati wa kuijenga Tanzania mpya, nina imani kubwa sana Mungu wetu atatusaidia, mwaka 2019 mengi mazuri yatafanyika, kikubwa ni mshikamano wetu sote Watanzania.

“Niwaombe Watanzania wote wa rika zote, wa dini zote, wa makabila yote, mshikamano waliouonesha kwa mwaka 2018 katika Serikali, wauoneshe tena mwaka 2019, na ikiwezekana wauoneshe zaidi na zaidi kwa kutanguliza zaidi uzalendo na Utanzania wetu, tutafanikiwa, Mungu ni mwema, Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki Watanzania wote na Mungu ubariki mwaka 2019,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles