26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

John Legend, Chrissy watarajia mtoto

John Legend na mkeNEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, John Legend na mke wake, Chrissy Teigen, wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.

Wawili hao walifanikiwa kufunga ndoa Septemba 2013, lakini hawakufanikiwa kupata mtoto kwa kipindi kirefu.

“Tuna furaha kubwa kutangaza kwamba tunatarajia kupata mtoto wetu wa kwanza, sio kazi rahisi lakini tunamshukuru Mungu kwa kusikia kilio chetu, tunatarajia kuongeza familia yetu,” alisema Chrissy kupitia akaunti yake ya Instagram.

Mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 29, amesisitiza kuwa yeye na mume wake walikuwa na kipindi kigumu walipokuwa wakitafuta mtoto ndani ya miaka mitano iliyopita.

“Tumepata misukosuko mingi ndani ya miaka mitano iliyopita juu ya kutafuta mtoto, lakini kwa sasa tunajiandaa kulea,” alieleza kwa furaha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles