28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Drake ashangaza mashabiki, anunuliwa pete

drake na futureLOS ANGELES, MAREKANI

MASHABIKI wa muziki nchini Marekani, wameshangaa kitendo cha msanii wa hip hop, Nayvadius Wilburn ‘Future’, kumnunulia msanii mwenzake, Aubrey Graham ‘Drake’ pete ya dhahabu.

Mashabiki wengi wamedai kuwa ni bora angemnunulia saa, cheni na vitu vingine kuliko kumnunulia pete, kwa kuwa inatafsiri vibaya kwa mwanaume.

Wawili hao wa sasa wanafanya kazi za muziki pamoja, hivyo Future amesema kuwa amefanya hivyo kwa kuwa kuna wimbo wao unaitwa ‘Big Rings’ ambao upo kwenye albamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la ‘What a Time to Be Alive’.

Hata hivyo, Drake ameonekana kufurahia pete hiyo ambapo aliamua kuweka picha wakiwa pamoja na kusema kuwa; “asante sana, pete kubwa kutoka kwa kaka Future,” alisema Drake.

Albamu yao kwa sasa inaonekana kufanya vizuri katika soko la Billboard, ambapo mpaka sasa imefanya mauzo ya zaidi ya nakala 330,000 kwa wiki moja ya kwanza.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles