30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Polisi laipongeza SGA kwa kuwajali wafanyakazi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Ulinzi nchini SGA Security, imepogezwa na Jesi la Polisi nchini kwa namna inavyowahudumia wafanyakazi wake.

Pongezi hizo zimetolewa leo Jumatatu, Desemba 21, na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai wakati akiwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu katika kampuni hiyo.  

Kamanda huyo amesema jitihada za SGA katika kujali masilahi ya wafanyakazi ilisababisha kampuni hiyo kupata tuzo ya kampuni bora ya ulinzi iliyo na vifaa vya kutosha na inaamnika zaidi yaani Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020 award wakati wa Tuzo za Chaguo la Mteja (Tanzania Consumer Choice Awards) Jijini Dar es Salaam hivi karibuni na inadhihirisha imani ya wateja kwa SGA.  

Kamanda Kingai ametoa wito kwa makampuni mengine ya ulinzi yaige mfano wa SGA Security na namna inavyoendesha shughuli zake.

Amesema alipata nafasi ya kushuhudia namna SGA inaendesha shughuli zake na alifurashishwa na namna kampuni hiyo imewekeza katika teknolojia ya kisasa ikiwemo magari yanayotumiwa kusafirisha vitu vyenye thamani, jambo ambalo limefanya kampuni hiyo iendelee kuongoza katika sekta hiyo.

Amesema kinachofanywa na kampuni hiyo kinaendana na maono ya Rais John Magufuli ya wawekezaji kuwapa wafanyakazi wao kipaumbele.  

“Niwapongeze wafanyakazi wote waliotimiza miaka 20 na zaidi kazini ambao mnajiunga na Kilabu maalumu inachojulikana kama Club 20, jambo ambalo ni nadra kwa makampuni binafsi ya ulinzi, niwakumbushe tu kwamba siri ya mafanikio ni kujituma, nidhamu na weledi katika utendaji wa kazi,”amesema.

Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Ramadhan Kingai (kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa wafanyakazi waliohudumu katika  kampuni ya SGA Security kwa miaka mingi. Tuzo hiyo ilitolewa wakati  wa hafla ya mwisho wa mwaka kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu.

Miongoni mwa waliotunikiwa ni pamoja na, Clifton Desouza aliyeitumikia kampuni hiyo kwa miaka 42.

Alitumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa makampuni yote ya ulinzi kufuata sheria na miongozo inayotolewa na Jeshi la polisi na kuwataka pia watumie jeshi hilo katika zoezi la kuwapata walinzi wazuri ambao wana sifa njema na wasio na rekodi ya uhalifu.

“Mameneja rasilimaliwatu wana jukumu la kutunza kumpukumbu za wafanyakazi vizuri na zinajitosheleza ikiwemo kitambulisho cha taifa na taarifa za wadhamini wao,” alisema na kuongeza kuwa kumekuwepo kesi za walinzi kukabidhi nyaraka feki na kumbukumbu feki za wadhamini na baadaye kufanya uhalifu na kukimbia.

Shughuli hiyo ya kuwatunuku wafanyakazi ilifanyika katika matawi yote ya SGA  Security nchi nzima huku Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Eric Sambu akielezea kuwa shughuli hiyo ya kuwatambua wafanyakazi waliohudumu kwa zaidi ya miaka 20 hufanyika kila mwaka na wao hujiunga katika Club 20.

Amesema hadi sasa Club 20 ina zaidi ya wanachama 240 na wanazidi kuongezeka na kudhihirisha kuwa wafanyakazi hao wana malengo ya kufanya kazi na kampuni hiyo hadi wakati wa kustaafu kisheria.

Ameongeza kuwa SGA ina wafanyakazi zaidi ya 6,000 nchi nzima huku Meneja Rasilimali watu, Ebenezer Kaale akisema siri ya mafanikio ni jinsi wamekuwa wakiwajali wafanyakazi wao.

“Tunaamini kuwa tukiwajali basi nao watawajali wateja zaidi. Huwa tunawachunguza vizuri kabla ya kuwaajiri, tunawapa mafunzo ya mara kwa mara na pia kuwapa motisha mara kwa mara,” amesema Kaale.

SGA Security inatoa huduma mbalimbali ikiwemo za ulinzi, alarm, huduma za fedha, ulinzi wa kielektroniki, huduma ya kusafirisha mizigo na huduma nyingine.

SGA pia inajivunia kuwa kampuni pekee yenye cheti cha ISO18788 (Security Operations Management System). Pia ina ISO 9001: 2015 na ISO 45000:2018 (Occupation Health and Safety).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles