29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Jengeni kwenu kuondoa aibu mnapopata matatizo-Padri

Na Anna Ruhasha, Sengerema  

Watoto wenye uwezo wa kuwatunza wazazi wao au walezi wamekumbushwa kufanya hivyo ili kujitengenezea baraka na neema kwa Mungu kupitia kazi ya mikono yao wakiwa hapa duniani.

Hatua hiyo pia imeelezwa kuwa itasaidia kupunguza aibu kwa watoto wanaoishi na kufanyakazi mijini pindi wanapopata matatizo na kuletwa kijijini walipozaliwa.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Septemba 16, 2021 na Padri George Nkombolwa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyantakubwa Jimbo la Geita wakati akibariki ufunguzi wa nyumba baada ya watoto kuwajengea wazazi wao katika Kijiji na kata ya Nyamtelele wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Katika mahubiri ya Misa hiyo Takatifu kabla ya kubariki ufunguzi wa nyumba hiyo, Padri Nkombolwa amesema huo ni mfano wa kuigwa kwa wale ambao wanashindwa kuwajengea nyumba wazazi wao ilihali kwamba wanavipato na mwisho wa siku panapotokea shida kwao wanaanza kuhangaika kitendo kinacho mchukizi Muumba wao.

“Niwapongeze watoto wa familia hii mkiongozwa na kijana Manoti ambaye amekuwa akijushulisha mara kwa mara na baada ya Mungu kumbariki kipato akaona awajenge wazazi wake hii ni neema na baraka kwake na kwa ndungu zake waliomuunga mkono, hili liwe funzo kwa mliopo hapa wafanyabishara kama haujajenga kwenu kajenge uenda kuna wakati hampigi hatua sababu hamjapatendea haki kwenu na wazazi wako haujawasaidia.

“Hivyo niwasihi kwamba ambao mko mijini mnafanyakazi jengeni kwenu ili kuondoa aibu pindi mnapofikwa na matatizo huko mjini na kupelekwa vijijini,” amesema Padri Nkombolwa.


Baadhi ya wananchi wilayani humo akiwamo, Juma Masoud amepongeza hatua hiyo na kusema ni moja ya somo kwa wale ambao wanashindwa kuwatenezea mazingira mazuri ya kuishi wazazi wao licha ya kuwa na uwezo huo.

“Huu ni mfano wa kuigwa unakuta Kuna watoto matajiri wazazi wao waliuza mashamba kwa kuwasomesha lakini ukifika kwao unatoa machozi na wengi wao niwale wenye pesa, wengi wanakufa uko makazini wanapoletwa vijijini  hakuna nyumba wakati alikuwa na nafasi nzuri ya kujenga kwao tumejinfunza,”

amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles