27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake watakiwa kuongeza kasi michezoni

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wanawake wametakiwa kuongeza kasi ya ushiriki wa michezo ili kwenda na wakati uliopo ikiwamo kunufaika na fursa zilizopo katika sekta hiyo kama ilivyo kwa wanaume.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 16, 2021 na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Michezo Vyuo Vikuu Tanzania(TUSA), Sophia Nchimbi wakati akitoa mada katika kongamano la wanamichezo wanawake lililofanyika ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kongamano hilo ambalo ni maandalizi kuelekea katika Tamasha la Michezo la Wanawake Tanzanite, linaonza leo hadi Jumamosi, limeshirikisha wadau mbalimbali wa michezo Tanzania.


Akitoa mada, Sophia amesema ushiriki wa wanawake katika michezo umekuwa ukipanda na kushuka, hivyo inahitajika nguvu zaidi ili kufikia walipo wanaume.


“Hatushindani na wanaume lakini tunaweza kufikia walipo kimichezo, ukiangalia kwa sasa ushiriki wa wanawake katika michezo ni asilimia 30, tunahitaji kuongeza kasi wanawake,” amesema.


Ameeleza kuwa zipo changamoto nyingi zinazomzuia mwanamke kushiriki michezo lakini moja wapo ni ile ya kuona baadhi ya michezo ni ya wanaume.


“Lakini pia kikwazo kingine ni wanaume, kwa sababu mwanamke anapoolewa anakuwa anamsikiliza mume wake, ila hilo tunatakiwa tujitahidi tulishinde kwa kuwashirikisha kile tunachotaka kufanya,” ameeleza Sophia.

Baadhi ya wanamichezo wanawake wakisikiliza mada katika ongamano hilo.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas ambaye alikuwa mgeni rasmi, amevitaka vyama vya michezo vya wanawake kutumia vizuri tasnia ya habari kujitangaza.


“Pamoja na changamoto nyingi mnatakiwa kutumia vyombo vya habari kujitangaza, kumekuwa na tatizo katika eneo hilo la kujitangaza,” amesema.


Naye Katimu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, amesema Tanzania bado haijapika hatua kubwa ya kuifanya michezo kuwa taaluma(proffesional) hivyo ni jukumu la wanawake hao kupambana.


“Tanzania bado tunachechemea katika kuwa proffesional kwa sababu bado kuna uvunjwaji wa kanuni na kutokujiamini,lakini taratibu tutafika, ” amesema Neema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles