Jay-Z ashtakiwa kutumia nyimbo za Prince

0
572

jayz

NEW YORK, MAREKANI

FAMILIA ya marehemu Prince Nelson ambaye alikuwa nyota wa muziki nchini Marekani, imemshitaki rapa Jay Z kwa madai kwamba anatumia nyimbo za marehemu bila ruhusa kutoka ndani ya familia hiyo.

Inasemekana kuwa Prince awali alikuwa anafanya kazi chini ya Jay Z, lakini baadaye aliondoka, hivyo kulikuwa na kazi ambazo alizifanya chini ya lebo ya rapa huyo ya Roc Nation, lakini Jay Z anaonekana kuzitumia nyimbo hizo tangu Juni mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, familia ya marehemu imepanga kutaka kumchukulia hatua rapa huyo kutokana na kutumia kazi hizo kwa kipindi chote bila ruhusa yao.

Hata hivyo kampuni hiyo ya Jay Z imedai kuwa kulikuwa na makubaliano baina ya kampuni hiyo na Prince kwa maneno ya mdomo pamoja na maandishi ya pande zote mbili katika matumizi ya kazi hizo.

Nyimbo ambazo zinatumika na mtandao wa Jay Z ni pamoja I Wanna Be Your Lover, Little Red Corvette, Cream, Purple Rain, Controversy, Pop Life.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here