29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mariah amdai Cannon matumizi ya watoto

mariah-carey

NEW YORK, MAREKANI

MSANII wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey, amemtaka mume wake wa zamani Nick Cannon kutoa dola za Kimarekani milioni 6 kwa mwaka sawa na zaidi ya bilioni 12 za Kitanzania kwa ajili ya huduma kwa watoto wao.

Wawili hao walifanikiwa kupata watoto mapacha ambao kwa sasa wana umri wa miaka mitano, lakini wawili hao waliachana mapema mwaka huu hivyo Mariah amemtaka Cannon kuwa anatoa dola milioni 6 kwa mwaka kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao ambao wanajulikana kwa majina Monroe na Moroccan.

Mrembo huyo amesema kuwa watoto hao wapo kwake kwa sasa kutokana na umri wao kuwa mdogo, hivyo baba wa watoto anatakiwa kutoa fedha hizo za matumizi kwa mwaka.

“Cannon anatakiwa kutoa dola million 6 kwa mwaka kwa ajili ya huduma kwa watoto na kama itakuwa ngumu basi anaweza kutoa dola 100,000 katika kila mwezi,” alisema Mariah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles