28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

JATA yawataka wachezaji kufanya mazoezi ya viwango

Sharifa Mmasi, Mtanzania Digital

UONGOZI wa Chama cha Mchezo wa Judo Tanzania ( JATA), umewataka wachezaji wa klabu zote nchini, kuendelea kufanya mazoezi yenye viwango vya hali ya juu lengo ni kujiweka fiti tayari kwa mashindano ya klabu.

Mashindano hayo yanayohusisha  klabu mbalimbali za Tanzania, yamepangwa kufanyika Oktoba 10-11 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtanzania Digital, Katibu Mkuu wa JATA, Innocenta Malya amesema mashindano hayo yataonyeshwa mubashara kupitia runinga ya Azam.

Aidha, amesema lengo la mashindano hayo ni kusaka wachezaji wenye viwango kwa ajili ya kuunda timu ya taifa ya Tanzania itakayoshiriki michuano ya Afrika Mashariki 2022 nchini Uganda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles