Mwandishi wetu,Arusha
Mkoa wa Arusha , Wananchi wa jamii za kifugaji na Wahadzabe wametakiwa Kujitokeza kupata chanjo ya Uviko-19 baada ya jamii hizo kuwa nyuma katika awamu ya kwanza.
Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 Mkoa Arusha Dk Willson Boniface amesema wilaya za Ngorongoro na Longido zipo nyuma katika chanjo awamu ya kwanza sasa mkazo wa umeongezwa katika elimu kwani awamu ya Kwanza kulikuwa na upotoshwaji juu ya Chanjo.
“Tumeanza kutoa elimu ya Chanjo Kupitia viongozi wa Mila , makanisani na kwenda manyumbani lengo kuhakikisha elimu inatolewa juu ya umuhimu wa chanjo na itabaki hiari kuchanja”Amesema
Hata hivyo amesema Mkoa katika awamu ya kwanza uliofanya vizuri kwa kuchanja 47,950 kati ya Chanjo 50,000 zilizopokelewa.
Mratibu wa chanjo ya Uviko-19 mkoa Arusha Dk Willson Boniface amesema zoezi la Chanjo awamu ya pili limeanza na wanatarajia Wakazi wengi kujitokeza.
Amesema katika awamu ya kwanza, Jiji la Arusha ndio limeongoza Kwa kuchanja watu wengi zaidi likifatiwa na Halmashauri ya Arusha Dc na Halmashauri ya Meru..
Amesema awamu ya kwanza jamii za kifugaji zilikuwa nyuma kutokana na upotoshwaji uliokuwepo lakini Sasa hali imeanza kuwa tofauti kutokana na elimu inayotolewa majumbani,Kwa viongozi wa Mila na makanisani.
Amesema Mkoa Arusha tayari umepokea chanjo nyingine 39,809 aina ya sinopharm ambazo mtu atapata chanjo Mara mbili.
“Baada ya kupokea chanjo za pili aina ya sinopharm Sasa elimu tunaendelea kutoa na watu wameendelea kuchanja”amesema
Amesema katika awamu ya pili watu watapata chanjo mara mbili tofauti na chanjo ya awamu ya kwanza ya Johnson & Johnson
” Tunaomba watu wajitokeze kwani chanjo zipo salama kabisa na safari hii chanjo itakuwa ni mara mbili”amesema.
Hivi karibuni shirika la kimataifa la journalist for human Rights (JHR) Kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari kusaidia jamii za kifugaji na pembezoni (MAIPAC) ilitoa elimu Kwa wanahabari katika jamii hizo kutoa elimu ya Chanjo hasa kutokana na jamii hiyo kuwa nyuma.