23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kuondoa baadhi ya tozo kwenye elimu

Na Upendo Mosha,Moshi

WADAU wa Elimu, ikiwemo Taasisi za dini katika Mkoa wa Kilimanjaro, wameiomba serikali kuondoa baadhi ya tozo na kodi ambazo zimekuwa changamoto katika shule hizo, hatua ambayo itawasaidia kuendeleza juhudi za serikali katika utoaji wa huduma ya elimu bora nchini na kukuza sekta hiyo.

Ombio hilo lilitolewa jana na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya Mtakatifu, Papa Yohani Paulo wa pili, Lombeta, Padre Dk. Aidan Msafiri,wakati akizungumza katika mahafali ya 43 ya shule hiyo, iliyopo wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Amesema ni vema serikali ikaandaa utaratibu maalumu wa kuziwezesha shule hizo kwa kuondoa kodi na tozo hizo kwani wamekuwa wakitoa huduma kwa jamii ikiwemo kusaidia watoto yatima na wale waishi kwenye mazingira magumu na kwamba hazipo kibiashara.

“Tunaiomba serikali ikaangalia upya uamuzi wa kuzilipisha kodi shule zinazomilikiwa na taasisi zetu zote za dini ikiwemo hizi za Umoja wa Mapadre Wa Jimbo Katoliki Moshi, (UMAWATA) kwani zilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu na malezi bora kwa watoto wa wananchi wote na wale wasiokuwa na kipato kikubwa,” amesema Padre Msafiri.

Aidha, amesema ada ndogo zinazolipwa na wanafunzi hutumika kulipa waalimu na watumishi wengine mishahara ikiwa ni pamoja na kununua chakula kwa ajili ya wanafunzi na kwamba serikali kuzitaka shule hizo kulipa kodi inalengo la kukwamisha utoaji wa huduma hizo kwa jamii.

“Huduma hii sio biashara Ila ni namna ya kuwezesha binadamu kujitegemea na kuwa na maarifa na awe na maendeleo endelevu na ajenge jamii yake …inchi na kanuni na Sheria zake ambazo hatuzipingi lakini kanisa no mdau mkubwa wa elimu na afya…hivyo kuendelea kutoza Kodi no kuinyima jamii haki yake maana shule zitashindwa kujiendesha,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya shule za sekondari zinazomilikiwa na Umoja wa Mapadre jimbo katoliki Moshi (UMAWATA), Padre Faustine Furaha, ameiomba serikali kuangalia namna ya kutofautisha shule zinazofanywa biashara na zile ambazo zimekuwa zikitoa huduma ili kuondoa tozo na kodi hizo.

“Shule zetu hazifanyi biashara tunatoa huduma hivyo tunaiomba serikali itofautishe Kati ya shule zinazofanywa biashara na zile ambazo hatufanyi biashara ….sisi na ni wadau na hatuna tofauti na shule za serikali, tunatoa huduma Kama wanazotoa wao Ila tunaonekana sisi Kama watoto wa kambo,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo, Cleophas Bossi, amesema serikali kuzitaka shule hizo kulipa kodi ni pigo kubwa kwa jamii kwani kunauwezekano mkubwa wa kushindwa kujiendesha na kufikia malengo ya serikali ya utoaji wa elimu bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles