24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

‘JAMII IWAJIBIKE NA MALEZI BORA YA WATOTO’

 

Na ASHA BANI

-DAR ES SALAAM

JAMII imeaswa kuwajibika katika malezi bora ya watoto wao hasa wa kike ili kuepukana na mimba za utotoni na kukatisha ndoto za watoto hao.

Hayo yalielezwa jana na mgeni rasmi ambaye ni mmoja kati ya wazazi waliofika kuhudhuria mahafali hayo  aliyejitambulisha kwa jina la Tusekile Mwaisabila katika mahafali ya nane ya Shule ya Msingi na Awali ya Andrew’s

Tusekile alisema imefika wakati sasa wazazi wasiwe ni sehemu ya kulalamika kuhusu malezi ya watoto hasa wa kike bali wawe ni moja ya majukumu yao hasa kuwalea katika maadili mazuri na misingi imara ya dini.

Alisema endapo mtoto atalelewa katika misingi bora ya dini, ni lazima atakuwa mwenye heshima na asiyeweza kujiunga na makundi mabaya yenye kuchafua taswira yake katika masomo.

Hivyo aliwaasa wazazi wawe na mfano mzuri katika kushirikiana na walimu ambao wamekuwa wakiwalea watoto wao kuanzia asubuhi hadi jioni wanaporejea majumbani mwao.

Lakini pia aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa hatua iliyofika kuanzia ilipoanzishwa kwake  mwaka 1998 hadi ilipofikia leo na kuwa na idadi ya wanafunzi 230.

Akizungumza mara baada ya mahafali hayo, Mkurugenzi wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Anna Mwambije, alisema kuendesha shule si jambo rahisi lakini yeye akiwa kama mwanamke ameweza.

Alisema ameanza mwaka 1998 akiwa amepanga nyumba kwa mtu lakini kwa sasa anamiliki jengo lake mwenyewe.

Alisema kutokana na juhudi binafsi zinazoonyeshwa na wazalendo katika kuendesha shule binafasi ni vyema Serikali ikaimarisha ushirikiano uliopo.

“Sisi wamiliki wa shule binafsi tuna mchango mkubwa katika familia, hivyo tunapaswa kuangaliwa na Serikali kwa jicho la tatu na kusaidiwa mambo mbalimbali ikiwemo hata ambavyo wanasaidia katika shule za Serikali na sisi tuweze kuvipata, mfano madawati hata mimi hapa nina uhaba wa madawati pia,” alisema.

mwisho

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles