26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

ANGELINA: SINA FURAHA KUKAA BILA MPENZI

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa filamu za Hollyhood, Angelina Jolie, amekuwa na wakati mgumu tangu alipoachana na mpenzi wake, Brad Pitt mwaka jana, hivyo amedai hana furaha kuishi bila mpenzi hata kama ana fedha za kutosha.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 42, aliliambia Gazeti la Telegraph la nchini Uingereza kwamba, amekuwa na wakati mgumu kuishi bila mpenzi, hivyo anakosa furaha kabisa.

“Huu ni wakati wangu mgumu sana katika maisha yangu, hata kama nina fedha, lakini kuishi bila ya mpenzi ni jambo ambalo halielezeki, nimekuwa nikiishi na wanangu kwa kipindi cha mwaka sasa, lakini bado sifurahii maisha.

“Hakuna kitu kizuri ambacho ninakifanya nikawa na furaha hasa nikikumbuka kuwa nipo peke yangu, nikiwa mitaani ninaonekana kama nina furaha lakini ukweli ni kwamba ninajikaza mbele za watu ila ninaumia sana,” alisema Angelina.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles