31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

LIL WAYNE KUPUMZIKA MUZIKI

CHICAGO, MAREKANI

RAPA Lil Wayne, ameruhusiwa kutoka hospitalini na kutakiwa kupumzika muziki kwa wiki mbili ili hali yake iweze kuimarika.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 34, alikutwa chumbani kwake wiki iliyopita akiwa amepoteza fahamu, hivyo alikimbizwa hospitalini kwa matibabu, lakini jana aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, msanii huyo anatakiwa kupumzika wiki mbili bila ya kufanya kazi yoyote ya muziki ili hali yake kuwa sawa.

Rapa huyo amedai kwa mara ya kwanza ataonekana kwenye tamasha la Stage AE, linalotarajiwa kufanyika Septemba 23, huko mjini Pittsburgh nchini Marekani.

Si mara ya kwanza kwa Lil Wayne kukutwa amepoteza fahamu, msanii huyo amekuwa akipata tatizo hilo kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kifafa tangu akiwa na umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles