Izzo Business hajui idadi ya mashabiki wake

0
678

IzzomNA CHRISTOPHER MSEKENA

LICHA ya kujivunia kuwa na mashabiki wengi wanaofuatilia muziki wake, lakini msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Emanuel Simwinga ‘Izzo Business’ hajui idadi kamili ya mashabiki wake hao.

Msanii huyo anayejihusisha na biashara mbalimbali tofauti na muziki ikiwemo ya mavazi, alisema tangu alipoanza muziki anaona mafanikio yake makubwa yanatokana na idadi kubwa ya mashabiki wake ingawa hajui idadi kamili ya mashabiki hao.

“Nashukuru napata fedha za kubadilishia mboga ambazo naamini zinatokana na mashabiki wangu kupitia muziki na mambo mengine ninayofanya kupitia muziki,’’ alieleza Izzo.

Aliongeza kwamba kwa sasa anaendelea kujiandaa na maonyesho mbalimbali ya kutangaza nyimbo zake mpya baada ya uchaguzi kuisha.

“Nina wimbo mpya nimeutambulisha hivi karibuni naamini utaanza kupendwa licha ya watu wengi kuangazia zaidi kwenye siasa lakini najiamini ndiyo maana nimetoa wimbo huo kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi ambapo wasanii wengi wanaangaika kuwanadi wagombea nafasi mbalimbali katika siasa,” alieleza msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here