25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 26, 2022

Kampeni yawakutanisha Juma Nature, Rich One

Rich & NatureNA MWANDISHI WETU

WASANII Juma Nature na Rich One waliowahi kuwika katika kundi la TMK Wanaume Halisi na kisha kutengana wamejikuta wakiimba pamoja katika kampeni za kumnadi mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.

Juzi wasanii hao walipanda katika jukwaa la Uwanja wa Mashujaa mjini Moshi na kuimba pamoja nyimbo mbalimbali walizowahi kushiriki wakiwa katika kundi lao la pamoja huku mashabiki wao wengi wakiendelea kuhoji umoja wao huo wakati walishatengana.

“Kweli siasa ina mambo, hawa jamaa walikuwa hawapatani, walitengana katika kundi lao la Wanaume Halisi baada ya kutoka TMK Wanaume leo kwenye siasa wapo pamoja, kweli siasa ndiyo kila kitu,” alisikika mmoja wa wadau wa muziki aliyejitambulisha kwa jina la Juma Maumba.

“Rich One aliwahi kuwika na wimbo wa ‘Pesa’ na Juma Nature aliwika na nyimbo nyingi na bado jina lake lipo juu katika sanaa ya muziki, mimi nawatakia maafanikio lakini ushirikiano wao kama wamerudi na wamepatana uwe hivyo hata baada ya uchaguzi maana kundi lao la Wanaume Halisi linawahitaji wote,”  alieleza mdau mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Muzda Mkanwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,404FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles