LONDON, ENGLAND
KOCHA wa Tottenham Spurs,Jose Mourinho amekiri wazi itakuwa ngumu kwa timu hiyo kurejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Mourinho ametoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kusukumwa nje ya michuano na RB Leipzig kwa jumla ya mabao 4-0, katika michezo miwili ya hatua 16 bora ya michuano hiyo.
Spurs ilikubali kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza, kabla ya kubugizwa mabao 3-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa juzi nchini Ujerumani.
Mkufunzi huyo raia wa Ureno ameiongoza Spurs kucheza michezo sita bila ushindi katika michuano yote hadi sasa.
Timu hiyo inashika nafasi ya nane katika msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 41, pointi saba nyuma ya Chelsea inayoshika nafasi ya nne ikiwa na pointi 48.
Mourinho atakuwa na shughuli nyingine pevu ya kukiongoza kikosi chake kusaka ushindi dhidi ya timu yake zamani, Manchester United utakaopigwa Jumapili.
Timu hiyo hiyo inakabiliwa na lundo la majeruhi kwa wachezaji wake muhimu akiwemo nahodha wao, Harry Kane.
“Pamoja na kikosi tulicho nacho kwa sasa itakuwa ngumu sana, “alisema Mourinho.
'Kila timu ulimwenguni ingepambana na wachezaji wao watano au sita muhimu kukosekana,kwa hivyo hiyo ni shida kubwa.
“ Najua timu yetu itaboresha moja kwa moja msimu ujao na wachezaji hawa kurudi, lakini tunajua lazima tuiboresha katika maeneo mengine.
"Akili wachezaji wanajaribu kuunda motisha zao na watatoa kila kitu wakati mwingine lakini sio rahisi kwao. '