28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Irene Uwoya; Mrembo hatari jikoni asiyependa kufua

Irene UwoyaNA KYALAA SEHEYE HANCHA

UHALISIA anaouvaa pale anapokuwa mbele ya kamera unamfanya awe nyota mkali wa filamu kwa mashabiki zake, huyu ni Irene Uwoya ambaye hashidwi kufanya lolote lile anapopewa mwongozo wa filamu yaani Script.

Diva huyu wa filamu za kitanzania ni mama wa mtoto mmoja anayeitwa Krish, aliyezaa na staa wa soka nchini Rwanda, Hamad Ndikumana, ambaye waliachana muda mrefu uliopita.

Irene Uwoya ni zao lililotoka kwa msanii Vicent Kigosi ‘Ray’, hivyo alipotambulishwa mbele ya mashabiki na kuuzoa ustaa, ustaa haukubalidisha tabia yake ya ucheshi na kutokuwa na dharau.

My Style, wiki hii imemdondosha mkali huyu wa filamu ili kufahamu mengi ambayo huwenda ulikuwa huyafahamu kutoka kwake akiwa ndani na nje ya tasnia ya filamu. Fuatilia mazungumzo yetu..

My Style: Kwa ufupi waambie mashabiki zako, Irene Uwoya ni nani?

Irene: Mimi siwezi kujiongelea ila watu wanaokaa na mimi karibu wanaweza wakawa na majibu mazuri zaidi yangu ila ninavyojijua mimi ni mtu mpole, nina upendo na kila mtu hata huruma pia ninayo na ni mwepesi wa kulia ninapokutana na jambo la kusikitisha.

My Style: Maisha yako yapo vipi?

Irene: Sipendi kabisa kuishi maisha ya kuiga. Kumfuatilia mtu anafanya nini ili na mimi nifanye, nipo hivyo kwa kuwa hata mimi sipendi kufuatiliwa kwenye mambo yangu.

My Style: Inawezekana mumeo alikuwa anakufuatilia sana ndiyo maana ukaachana naye, au kuna nini nyuma ya pazia?

Irene: Yapo mambo mengi ila hilo pia ni jambo lililochangia tuachane.

My Style: Ulikuwa ni mmoja kati ya wasanii wengi walioingia kwenye mchakato wa kutafuta Uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka jana, ulijisikiaje ulipokosa nafasi ya kuwa Mbunge kule Tabora?

Irene: Binafsi nilijisikia vizuri kwa sababu nilidhubutu. Mpaka sasa nina heshima kubwa ndani ya chama changu hata kwa wananchi pia. Vijana tusiogope kujaribu kufanya mambo makubwa.

My Style: Toka umeanza kufahamika ni muda mrefu sasa, umaarufu umekupa faida gani au ustaa wako unakusaidia vipi?

Irene: Umaarufu unasaidia sana hasa katika maisha haya ya mjini. Unaweza kuingia sehemu ukaheshimika kwa kuwa wewe ni msanii na muda mwingine unapata huduma kwa haraka zaidi tofauti na watu wengine.

My Style: Mbali na faida hizo za umaarufu wako, unakutana na usumbufu gani?

Irene: Usumbufu mkubwa ninaoupata ni ule ya kuzushiwa jambo kisa mimi ni staa, sipendi kwa sababu kuna mashabiki zangu wanauamini huo uzushi unao nipunguzia heshima.

My Style: Unapenda kufanya kazi gani ukiwa nyumbani?

Irene: Napenda sana kupika, mimi ni mpishi mzuri mno wa vyakula mbalimbali, nadhani hata aliyekuwa mume wangu analitambua hilo, ila sipendi kabisa kufua nguo.

My Style: Kwa kumalizia unawapa ushauri gani wasanii wenzako?

Irene: Tupendane na tuzidishe ushirikiano kwani naamini Tanzania tunaweza sana, kama tumeweza kuiteka Afrika Mashariki tunaweza kuwazidi Nigeria na Ghana ambao wapo juu kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles