33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kifafa kinavyotishia uhai wa Lil Wayne

Lil WayneNA BADI MCHOMOLO

MWISHONI mwa mwaka uliopita kulikuwa na habari zinazomhusu rapa Lil Wayne, kusumbuliwa na maradhi ya Saratani kwa muda mrefu hivyo ingekuwa ngumu kwake kumaliza mwaka ule bila kupoteza maisha. Hata yeye mwenyewe aliamua kuweka wazi kuwa ugonjwa huo umemtafuna kwa kiasi kikubwa na upo kwenye hatua za mwisho na za hatari.

Michoro iliyojaa kwenye mwili wake yaani Tatoo, ilifanya ugonjwa huo usionekana kirahisi mpaka mwaka jana ilipotoa taarifa kuwa ameshambuliwa kwa kiasi kikubwa na inawezekana asimalize mwaka ule lakini kwa kurda za Mungu ,rapa huyo mwenye miaka 33 amefanikiwa kuuona mwaka 2016.

Wakati mamilioni ya mashabiki zake wakidhani kifo cha rapa Lil Wayne kitatokana na Saratani, yeye mwenyewe anasema anaweza kufa kutokana na ugonjwa wa Kifafa ambao umekuwa ukimsumbua angali mtoto mdogo.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2012, Lil Wayne alishambuliwa na ugonjwa wa Kifafa hivyo kupoteza fahamu akiwa kwenye ndege, ambapo alipewa huduma ya kwanza na baadae kufikishwa hospitali na kupewa matibabu yaliyochukua muda wa siku mbili.

Hofu ya kutumbuiza kwenye majukwaa mbalimbali ilimjaa Lil Wayne, kwa kuwa alikuwa anahisi anaweza kuanguka akiwa jukwaani. Kutokana na ubora wake uliokuja baada na kufanya ngoma nyingi zilizotikisa chati za muziki duniani, alikuwa anapata maonyesho ya mara kwa mara na alilazimika kwenda na daktari kila anapopata mwaliko.
Aprili 2013, alipoteza fahamu kwa muda mrefu zaidi na kupelekea vyombo vya habari kutoa angalizo kuwa huwenda mashabiki wa msanii huyo wakampoteza kwani hali ilikuwa inatisha mno.

Tangu mwaka huo hali yake ilitengamaa mpaka mwanzoni mwa wiki hii ambapo Kifafa kilimshambulia tena akiwa kwenye ndege akitokea Wisconsin kwenda California, kikazi.

Rubani wa ndege hiyo alilazimika kutua kwa dharura kwa ajili ya kumkimbiza Lil Wayne hospitali, lakini baada ya kufika kwenye gari ya wagonjwa alipata fahamu na kugoma kupelekwa hospitali.

Msanii huyo alirudi kwenye ndege na kuendelea na safari, lakini dakika mbili baada ya ndege kupaa angani, rapa Lil Wayne alianguka tena na kupoteza fahamu hivyo madaktari waliamua kumfanyia matibabu ndani ya ndege.
Mara baada ya hali yake kukaa sawa, msanii huyo amedai kwamba ugonjwa huo kwa sasa unamtisha zaidi kuliko Saratani iliyodhaniwa kuwa ni tishio zaidi kwake.

“Nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani kwa miaka mingi japokuwa nimekuja kugundua miaka ya hivi karibuni, nilikuwa na wasi wasi wa kupoteza maisha yangu kwa Saratani lakini hali imekuwa tofauti hivi sasa nina wasiwasi na Kifafa kinaweza kupoteza maisha yangu.

Kuanguka na kupoteza fahamu ni tatizo kwa kuwa haujui utaanguka kwenye mazingira yapi, unaweza kuanguka jukwaani, ukapoteza fahamu ukiwa unaendesha gari au sehemu yoyote mbaya, kwa kweli inanitisha,” anasema aliandika Lil Wayne.

Kutokana na hali hiyo Lil Wayne analazimika kutembea na madaktari kwa ajili ya kumpa msaada popote pale ugonjwa huo utakapo mshambulia.

Tukutane wiki ijayo kwenye safu hii ya ‘Zaidi Ujuavyo’ kutaka kujua zaidi tuwasiliane kwa namba 0714107464 au [email protected]

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles