26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Ileje yatangaza motisha kwa walimu watakaofaulisha alama A

Na Denis Sikonde, Songwe

Wakati Mkoa wa Songwe ukipambana kutafuta mwarobaini unaosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu, wilaya ya Ileje kuanza, kutoa motisha kwa walimu watakofaulisha wanafunzi kwa kila somo kuanzia alama A wapewe motisha sambamba na kuwa na kauli mbiu ya kutokomeza sifuli kwa madarasa ya mitihani ya kitaifa.

Waratibu kata, wakuu wa shule za sekondari na walimu wakuu shule za msingi.

Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Mkoa wa Songwe, Michael Ligola, leo Februari 7,2022, wakati akizungumza na maafisa elimu, msingi na sekondari, Waratibu elimu kata, Wakuu na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo katika kikao cha kujadili mikakati ya kuongeza ufaulu ambapo wilaya ya Ileje imeshika nafasi ya mwisho kimkoa ikiwa na asilimia 56, kilichofanyika katika ukumbi wa Mother Land uliopo Itumba.

Ligola amesema ni wakati sasa halmashauri ya Ileje kuanza kutoa motisha kwa walimu na  wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo yao katika mitihani ya kitaifa.

“Matokeo yetu sio mazuri ila tumeanza mchakato wa kuona namna ya kutoa motisha kwa walimu ambao wanafunzi watafanya vizuri kwenye masomo yao kwenye mitihani ya kitaifa ya darasa la nne, la saba na kidato cha pili na cha nne hata kuanzia na kila alama A, kwa Sh 3,000,” amesema Ligola.

Ligola amesema ni jukumu la maafisa elimu kata kuwa na jukumu la kuzitembelea shule na kutatua changamoto zinazowakabili na si kusubiri viongozi wa wilaya na mkoa, ikiwepo kufuatilia wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika nakwamba hatosita kumchukulia hatua mratibu atakayewasilisha taarifa za wanafunzi wasiojuwa kusoma na kuandika.

Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Songwe, Christopher Senyamanza amesema moja ya changamoto inayoikanili wilaya ya Ileje ni uhaba wa walimu sambamba na uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika na kutoa wito kwa mkurugenzi wa halmashauri kuweka uwiano sawa kwa walimu kwa shule za msingi.

Upande wake Afisa Elimu sekondari wilaya ya Ileje, Gloria Kang’oma amewataka wakuu wa shule kutoa taarifa za kila mwezi kwa changamoto zinazoikabili, sambamba na waratibu kuwa na mkakati wa ufuatiliaji katika maeneo yao ya kazi mikakati ya ufaulu iweze kuleta mafanikio.

Nae Afisa Elimu msingi wilayani hapo, Fikiri Mguye amesema kutokana na changamoto zinazoikabili wilaya ya Ileje kufanya vibaya kwenye mitihani ya kitaifa, kulinganisha na wilaya zingine mkoani humo wanapaswa kuongeza bidii kusimamia ufundishaji, kwani mikakati hiyo wameainza toka Desemba, mwaka jana ambapo kufikia mwezi Julai, 2022, watakuwa wamemaliza changamoto zinazokwamisha ufaulu ili kwa matokeo ya mwaka 2023 Ileje ifanye vizuri.

Mwalimu mkuu shule ya msingi Kalembo, Fredy Mbughi, amesema licha ya mikakati ya kuongeza ufaulu, ameanza kuweka motisha kwa walimu kwa kupata chai shuleni kila siku za kazi na kama shule waamejipanga kufikisha asilimia 75 licha kuwa na changamoto ya uhaba wa walimu.

Desemba 29, mwaka jana ofisi ya idara ya elimu walifanya kikao cha mikakati ya kujadili changamoto ya kushuka kiwango cha ufaulu nakwamba cha leo ni kikao cha pili na afisa elimu mkoa na kuahidi kuwapa motisha wanafunzi watakaofanya vizuri kwenye masomo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles