29.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yachangia vifaa vya ujenzi shule ya Sekondari Kisarawe II

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital 

Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Machi 8, Kampuni ya simu ya Halotel imechangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyoo kwenye bweni la wasichana kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Kisarawe II iliyoko Wilaya ya  Kigamboni Dar es Salam.

Vifaa  hivyovilivyotolewa  vyenye thamani ya Shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 7, ni pamoja na tanki la maji la lita 5,000,Masinki manne ya kunawia mikono, malumalu (tiles) za ukutani na sakafu boksi 100, Saruji mifuko 30 na Mchanga lori moja.

Akizungumza na Waandisi wa Habari leo Jumatatu Machi 07,2022 Mkuu wa kitengo cha bidhaa na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Sakina Makabu amesema kuwa  wameona ni muhimu kuadhimisha siku hiyo kwa kuchangia  nyanja ya elimu kwa kuunga mkono juhudi za serikali.

“Sisi Kama Kampuni Kampuni ya  simu ya   Halotel tunaamini vifaa hivi tulivyotoa ni Muhimu katika kujenga na kuboresha mazingira ya Shule ya kusoma na kujifunza na hasa kwa ajili ya usafi wa wanafunzi wa kike ili waweze kujisikia vizuri pindi wawapo shule kujisomea,”amesema Sakina.

Amesema manufaa ya vifaa hivyo wanatarajia yatasaidia kuongeza usalama, utulivu na kuinua kiwango chao cha ufaulu.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule hiyo, Florentin Assenga, akipokea masada wa vifaa hivyo,  ameishukuru Kampuni hiyo kwa kutoa vifaa hivyo vitakavyosaidia kukamilisha mabweni matatu yaliyoanza kujengwa ili kuwawezesha wanafunzi hao kuishi shuleni hapo.

“Shule hapa tunachangamoto nyingi kwanza upatikanaji wa maji tulikuwa na tanki la lita 200 ambalo halitoshelezi mahitaji ya wanafunzi wote, lakini Kwa kutuletea hili la lita 5,000 walao litasaidia kupunguza baadhi ya changamoto,” amesema Assenga.

Aidha Assenga ameeleza Kuwa bado shule yetu  inahitaji misaada ya kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo ujenzi wa uzio Ili kuimarisha usalama wa masingira kwa watoto  wa kike.

Naye Afisa Tawala Kigamboni, Pendo Mahalu ameipongeza Kampuni hiyo Kwa kuonesha mfano mzuri katika kuchangia maendeleo ya nchi kupitia sera ya kurudisha sehemu ya faida Kwa Jamii (CSR).

“Tumefarijika kupokea msaada huu kutoka Kampuni ya haloteli,naamini vifaa hivi wanafunzi wa kike  walioko kidato Cha tano na sita katika kuboresha mazingira yao kiafya,” amesema Mahalu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles