21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

MAUWASA kutumia milioni 500 usambazaji wa maji mjini Maswa

Na Samwel Mwanga,Maswa

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa(Mauwasa)iliyoko wilayani Maswa mkoani Simiyu itatumia kiasi cha Sh 509,884,320 ili kukamilisha mradi wa usambazaji wa maji katika mji huo.

 Hayo yameelezwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias kwa waandishi wa habari waliotembelea mji wa Maswa kuona utekelezaji wa mradi huo.

Alisema kuwa mradi huo unajulikana  kama Uboreshaji Huduma ya Maji Maswa Mjini kwa Ustawi wa Taifa kwa Maendeleo katika kupambana na Maambukizi ya Uviko 19.

“Fedha za kutekeleza mradi huu zinatokana na fedha za Uviko 19 ambazo tulizipata kutoka Wizara ya Maji ikiwa ni sehemu ya fedha ambazo Rais Samia Suluhu alipewa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo,”alisema. 

Alisema  kazi zilizopangwa kutekelezwa kwenye mradi huo ni pamoja na Uchimbaji wa mtaro na kulaza bomba na kufikia urefu wa Kilomita 21.65, Ujenzi wa Vituo vinne vya kuchotea maji na Ujenzi wa chemba 10.

Mhandisi Nandi alisema hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 74  na unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu na utaongeza wigo wa Mamlaka hiyo kupata wateja wapya 1,000 na kunufaisha mitaa 10  ya mjini Maswa na vijij vitatu.

Ameitaja mitaa hiyo ni pamoja na Mitimirefu, Majengo, SolaMwabomba, SolaUnyanyembe, Uzunguni, Ujenzi, Jashimba, Ikungulyasubi, Majebele na Badabada.

Vijiji ambavyo vitanufaika ni pamoja na  Iyogelo,Buyubi na Matalambuli.

Baadhi ya wananchi waliipongeza serikali kwa kuwafikishia maji safi na salama kwenye maeneo yao.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutufikishia maji katika eneo letu kwani tangu tupate uhuru hatujawahi kuwa na maji safi na salama hivyo ni jambo la kuishukuru serikali yetu,” amesema Ashura Haji.

 Mkuu wa wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge amewataka wananchi kuitunza miradi hiyo sambamba na kutunza miundombinu ya maji na kuonya mtu yeyote ambaye atabainika kuihujumu atachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Nitoe wito kwa wananchi kuitunza hii miradi ya maji na miundo mbinu yake na mtu yeyote ambaye atabainika kuhujumu miradi ya maji atachukuliwa hatua kali za kisheria,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles