22.5 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa Utalii duniani

Na Mwandishi Wetu, Hispania

Tanzania imesaini rasmi mkataba wa kukubali  kuwa  Mwenyeji wa Mkutano Mkubwa wa Utalii  wa 65 wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya  Utalii Duniani  (UNWTO)  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 5 hadi 7, mwaka huu jijini Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro amesaini mkataba huo mbele ya Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvil, Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Madrid nchini Hispania.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Mawaziri wote wa Utalii wa Bara la Afrika pamoja, Wabobezi wa kutangaza utalii na Wataalamu  wa masuala ya utalii kutoka nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza mara baada ya hafla ya utiaji saini, Waziri Ndumbaro amesema mkutano huo  ni  fursa kwa Wadau wa utalii nchini Tanzania kujifunza na kubadilishana uzoefu mkubwa wa  kuendesha Sekta ya Utalii hususani katika kipindi hiki ambacho sekta ya utalii imeanza kuimarika baada ya kuathiriwa na janga la UVIKO-19.

“Tumepewa heshima kubwa ya kuwa wenyeji wa mkutano huu ambapo naamini utafungua milango ya vivutio vyetu vya utalii kujulikana Duniani kote,” amesema Dk. Ndumbaro.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UNWTO, Zurab Pololikashvil amesema ataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha Tanzania inaendelea kufanya vizuri katika masuala ya utalii huku akiahidi kuipa kipaumbele Tanzania katika miradi mingi inayofadhiliwa na Shirika hilo.

“Nimekuwa nikipata ushirikiano wa kutosha kutoka Tanzania kupitia Waziri, Dk.Ndumbaro, utiaji saini wa leo wa kuwa Mwenyeji wa mkutano huu ni mwanzo tu wa kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika masuala ya utalii,” amesisitiza Katibu Mkuu huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles