26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Historia ya Samuel Sitta 1942 – 2016

1Na Patricia Kimelemeta-DAR ES SALAAM

SAMUEL SITTA, Spika mstaafu wa Bunge la tisa aliyejulikana kama Spika wa viwango na kasi hatunaye.

Alifariki dunia alfajiri ya Novemba 7 mwaka huu akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa maradhi ya saratani ya tezi dume.

Taarifa za kifo chake zilitolewa na mtoto wake, Benjamin Sitta ambaye ni meya wa Kinondoni, Dar es Salaam.

‘THATS life’ ni neno la mwisho la Spika mstaafu Samuel Sitta baada ya kuambiwa na daktari wake ambaye alikuwa anamtibu nchini Ujerumani kuwa asingeweza kupona kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Kauli hiyo ilitolewa na Benjamin alipozungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao Masaki, Dar es Salaam jana, akimnukuu marehemu baba yake.

Alisema marehemu baba yake alikuwa amekwisha kujiandaa kwa kifo baada ya daktari wake kumwambia hivyo, jambo ambalo lilimfanya kufa kifo chema.

“Daktari aliyekuwa anamtibu alimwambia baba kuwa hawezi kupona, lakini alimjibu ‘that’s life’ na hakuendelea tena,” alisema.

Alisema katika kipindi cha uhai wake baba yake alishika nyadhifa mbalimbali, jambo lililomjengea umaarufu ndani na nje ya nchi.

Benjamin alisema Mzee Sitta alisimamia mambo mbalimbali yakiwamo haki na pale alipoamua kutetea jambo lake.

Alisema katika kipindi hiki cha msiba, familia imefarijika baada ya kuona kila mmoja anamzungumzia jinsi anavyomfahamu.

“Kila mmoja anasema lake katika kipindi hiki cha msiba, hii inaonyesha jinsi gani watu wanamvyomfahamu kutokana na misimamo yake anapoamua jambo lake liende,” alisema.

Alisema kuwa familia inamshukuru Rais Dk. John Magufuli na Ofisi ya Bunge kwa jinsi walivyokuwa karibu nao tangu anaumwa hadi kifo chake.

Benjamin alisema kuwa taarifa za msiba zilipowafikia, Rais Magufuli aliwasiliana nao na kuwapa pole, jambo ambalo liliwafariji.

Alisema kwa sasa wanasubiri ratiba ya mazishi kutoka serikalini na Ofisi ya Bunge kwa maziko Urambo Mashariki mkoani Tabora.

Menjamin alisema kamati ya mazishi ndiyo itakayotoa ratiba ya kuwasili  mwili  wa marehemu.

Viongozi mbalimbali walionekana nyumbani kwa marehemu Sitta, Dar es Salaam jana ambao ni pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Stigomena Tax, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na aliyekuwa Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles