29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Henry ampinga Wenger

KUTAKA fainali za Kombe la Dunia zichezwe kila baada ya miaka miwili ni ishara ya kuchoka kimawazo, kwa mujibu wa straika wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry.

Kauli yake hiyo ni kama ‘dongo’ kwa aliyekuwa kocha wake, Arsene Wenger, ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Akiwa ndiye mkuu wa maendeleo ya soka wa FIFA, Wenger amekuwa akishiriki kuipa nguvu kampeni ya Shirikisho hilo kutaka michuano ya Kombe Dunia iwe inarindima kila baada ya miaka miwili na si minne kama ilivyo sasa.

Henry ambaye ni Mfaransa mwenzake, anapingana naye akisema: “Hivi hawa (FIFA) huwa wanawauliza wachezaji kweli? Nilicheza mara nne Kombe la Dunia na mara tatu fainali za Euro, nilitoka huko nikiwa hoi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles