26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Dybala ang’oka kikosini Argentina

STAA wa Juventus, Paulo Dybala, ameondoshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kinachojiandaa kwa mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Qatar.

Awali, Dybala alihumuhishwa kwenye kikosi kitakachozivaa Paraguay, Uruguay na Peru mwezi kuanzia wiki ijayo lakini majeraha ya paja yamemzuia kucheza mechi hizo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliumia alipokuwa akiichezea Juventus katika mchezo walioifunga Sampdoria mabao 3-2, ambapo alifunga bao la kwanza.

Kutokana na majeraha hayo, ndiyo maana aliikosa mechi ya Jumatano ya wiki hii, siku Juventus ilipoifunga Chelsea bao 1-0.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles