22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Hatuna changamoto za kiuongozi Arusha-Kimanta

Na Janeth Mushi, Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, Idd Kimanta amesema anafurahishwa na umoja, mshikamano na upendo baina ya viongozi mkoani humo ambao umewezesha ufanye vizuri katika matokeo ya kidato cha nne na cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni.

Aidha, amesema hakuna changamoto yoyote ya kiungozi katika mkoa wa Arusha na kuwasihi viongozi hao kuendelea kushirikiana na watendaji mkoani humo ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Kimanta ametoa kauli hiyo jana Januari 20, kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Arusha (RCC), kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa umma, sekta binafsi, viongozi wa dini na vyama vya siasa,ambapo ameaema pale penye umoja na mshilamano wa viongozi lazima utekelezaji wa maendeleo uwepo na uonekane kama ilivyo sasa kwa mkoa huo.

Amesema anawapongeza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote za mkoa huo, kwa kushirikiana na wananchi wa maeneo yao kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa 126 kwenye shule mbalimbali za sekondari vinavyohitajika kwa mwaka huu katika wilaya zote za mkoa huo.

“Hatuna changamoto za kiuongozi mkoa wa Arusha, wote ni wamoja na ndiyo maana nasisitiza lazima umoja uwepo huwa najisikia simanzi ninaposikia mahali fulani kuna changamoto za kiuongozi inanikosesha raha, kwani kukiwa na shida ya kiuongozi kutakuwa na shida ya utekelezaji wa maendeleo hivyo kutakapokuwa na dosari turekebishe haraka.

“Nimefurahishwa na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kwa kazi nzuri ya kushirikiana na wananchi suala la ujenzi wa madarasa kwani mbali ya kung’ara na kwenye matokeo tumeshika nafasi ya pili kwenye sekta  ya lishe ikitanguliwa na Mkoa wa Kigoma, tuzidi kudumisha umoja, upendo na ushirikiano,” amesema Kimanta.

Aidha, ameagiza viongozi wote wa Mkoa huo kuanza maandalizi ya ujenzi wa miuondombinu ya shule za sekondari ili kuwezesha wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 wa elimu bora waingie bila kukwama sababu ya uhaba wa vyumba vya madarasa na samani zake.

“Hili nalo tunalifahamu sababu watoto walioanza mpango wa elimu bure wapo darasa la sita mwaka huu na wengi mno, hivyo mwaka 2023 watakua sekondari hivyo tujiandae na uongezaji madarasa, viti, meza, vyoo na mahitaji yote yanayohitajika na tuongeze hivyo kwa kasi kulingana na idadi yao, ili muda ukifika tusianze kukimbizana kama hatujuwi,” amesema Kimanta.

Kuhusu kodi amesema kila mwananchi au mfanyabiashara anayestahili kulipa kodi lazima alipe ili kuendeleza mradi ya maendeleo kufanyika bila kukwama na siyo suala la hiari.

Aidha, ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa huo kushirikiana kuhakikisha kila mwananchi anayestahili ulipaji wa kodi alipe bila kukwepa.

Kauli ya KImanta imekuja ikiwa ni siku chache tu zimepita taungu mbunge wa Arusha mjini, Mrisho Gambo kiunukuliwa na Vyombo vya Habar akilalamikia baadhi ya viongozi wa mkoa huo ikiwamo kutompa ushirikiano katika  utekezaji wa maendeleo ya wananchi wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles