32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

HATIMA YA LEMA KUJULIKANA JANUARI 4

Na JANETH MUSHI – ARUSHA


lemaHATIMA ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), inatarajia kujulikana Januari 4, mwakani.

Siku hiyo, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, itatoa uamuzi wa rufaa ya mawakili wa Serikali waliyokata kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliompa Lema dhamana.

Hata hivyo, uamuzi huo wa dhamana haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya nia ya kukata rufaa waliyoitoa mawakili hao wa Serikali.

Jana, mahakama hiyo ilipanga kusikiliza rufaa ya maombi ya dhamana ya Lema namba 126 ya mwaka 2016. Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Wakili Inoccent Njau, huku Lema akiwakilishwa na jopo la mawakili watano wakiongozwa na Peter Kibatala. Wengine ni Adam Jabir, John Mallya, Faraji Mangula na Sheck Mfinanga.

Jaji Salma Magimbi aliyekuwa anasikiliza rufaa hiyo, aliwataka mawakili wa Jamhuri kuwasilisha hoja zao za rufaa leo, huku mawakili wa Lema wakitakiwa kujibu hoja hizo kesho na Januari 2 mwakani, kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa rufaa hiyo Januari 4.

Awali, wakili Kibatala alisema kwa kuwa rufaa ya Jamhuri ilishawasilishwa mahakamani hapo, ni vema mahakama hiyo ikaanza kuisikiliza kwa kuwa kinachobishaniwa ni dhamana ya Lema.

“Rufaa yetu tunapinga uamuzi wa mahakama ya chini kukataa kutoa masharti ya dhamana, maana dhamana ilishatolewa, ila wakati hakimu anajiandaa kuitoa, mawakili wa Serikali walitoa notisi ya kutaka kukata rufaa.

“Tunasema mahakama ilikosea kuacha kuweka masharti ya dhamana wakati imeshampa dhamana, mahakama ilitafsiri vibaya maana ilipaswa kumpa Lema dhamana,” alisema Kibatala.

Lema anakabiliwa na kesi mbili za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Hakimu Kamugisha alimpa Lema dhamana ila kabla hajatoa masharti ya dhamana, mawakili wa Serikali, Paul Kadushi na Matenus Marandu, waliwasilisha kwa njia ya mdomo notisi ya nia ya kukata rufaa kupinga.

Wakati huo huo, upande wa Jamhuri umewasilisha notisi ya mdomo ya nia ya kukata rufaa,Mahakama ya Rufaa Tanzania kupinga uamuzi wa Jaji Dk. Modesta Opiyo wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumwongezea Lema siku 10 za kuwasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa hiyo ya maombi ya dhamana.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka huu nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na hadi wakati huo, anashikiliwa katika mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo, mjini Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles