29.7 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

RC ATOA WIKI MBILI WANANCHI WAJENGE VYOO

Na Mwandishi Wetu-LINDI


 

godfrey-zambiMKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, ametoa wiki mbili kwa wakazi wa Jimbo la Ruangwa kuhakikisha wanajenga vyoo kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.

Pamoja na hatua hiyo, Zambi amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Joseph Mkirikiti afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo Januari 15, mwakani na endapo atakuta kuna mkazi wa kijiji chochote hajajenga choo, basi atozwe faisi ya Sh 50,000 mara moja.

Kauli hiyo aliitoa jana wilayani hapa wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula wakati akiwasalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa azungumze na wakazi wa vijiji hivyo.

Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema wakulima wengi wamevuna korosho msimu huu na baadhi yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.

“Hili ni agizo la Serikali siyo langu binafsi, kwa hiyo ni amri halali. Kikilipuka kipindupindu naanza na Mkuu wa Wilaya kabla na mimi sijaulizwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais,” alisema.

Katika hatua nyingine, Zambi amewahimiza wakazi wa vijiji hivyo wapande miche ya mikorosho katika msimu huu wa kilimo pindi mvua zitakapoanza kwani iliyopo imekaa kwa zaidi ya miaka 50 na sasa haizai matunda ya kutosha.

“Mkoa wetu una mpango wa kubadilisha miti ya mikorosho kwani mingi ni ya zamani na imekaa kwa zaidi ya miaka 40 hadi 50 na hivi sasa haina tija kwenye mazao yake. Mti mzuri wa korosho unazaa hadi kilo 40, lakini hii iliyopo sasa hivi inatoa kilo 10 tu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles