24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA ‘SCORPION’ YAENDELEA KUUNGURUMA

Na WAANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


 

scorpionSHAHIDI wa pili na wa tatu katika kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu Scorpion, wameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam namna walivyopata taarifa za tukio hilo.

Wakitoa ushahidi wao jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Frola Haule kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Nasoro Katuga, shahidi wa kwanza ambaye ni mke wa Said Mrisho aliyetobolewa macho, Stara Sudi, alidai mahakamani hapo kuwa siku ya tukio alimkuta mumewe huyo akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili huku akiwa amefungwa bandeji.

“Kabla ya mume wangu kupelekwa Hospitali ya Mkoa ya Amana nilimkuta akiwa amejaa majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na alikuwa amefungwa bandeji na kisha kukimbizwa Hospitali ya Taifa,” alisema Stara.

Upande wake shahidi namba tatu ambaye ni mdogo wa mlalamikaji, Yahaya Kisukari, aliieleza mahakama hiyo kuwa mara tu baada ya kupata taarifa za kujeruhiwa kwa kaka yake huyo walipomfuata jina la kwanza alilowatajia lilikuwa ni la mtuhumiwa ambaye ni Scorpion.

“Mara tu baada ya kuwa nimefika kwenye eneo la tukio usiku ule Mrisho alinitajia jina la mlalamikiwa ambaye ni Scorpion kuwa ndiye aliyemdhuru,” alisema Kisukari.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Januari 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na mtuhumiwa amerejeshwa rumande.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, mshtakiwa ambaye ni mwalimu wa karate, alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu maeneo ya Buguruni Sheli wilayani Ilala.

Ilidaiwa mshtakiwa aliiba cheni ya dhahabu gramu 38 yenye thamani ya Sh 60,000, kibangili cha mkononi na Sh 331,000 pamoja na pochi, vyote vina thamani ya Sh 476,000, mali ya Said Mrisho.

Ilidaiwa kabla ya wizi huo, alimchoma na kisu tumboni, mgongoni na machoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles