Hans Poppe awabeza Yanga

0
781

Hans PoppeNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amewabeza wapinzani wao Yanga akidai kuwa kipigo walichokipata kutoka kwa timu waliyoidharau kimewaumbua.
Simba ndio walikuwa wenyeji wa mchezo huo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Yanga ilikubali kipigo cha bao 1-0.
Akizungumza na MTANZANIA mara baada ya kumalizika mchezo huo, Hans Poppe alisema maneno mengi yalisemwa juu ya kikosi cha Simba kuwa hakina uwezo wa kuifunga Yanga, lakini kilichotokea kila mmoja alishuhudia.
“Tuliambiwa sisi sio wapinzani wa Yanga kwa kuwa wanashindana na timu za kimataifa tuliona ni sawa, lakini kipigo kimewaumbua na kudhihirisha kuwa sisi ni bora na hawawezi kutufunga,” alisema.
Alisema timu hiyo sasa inajipanga kusaka matokeo ya ushindi katika mechi zilizobaki Ligi Kuu ambapo Jumamosi ijayo watakutana na Mtibwa Sugar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here