22.3 C
Dar es Salaam
Saturday, July 13, 2024

Contact us: [email protected]

Gurost Elmodo atikisa na ‘Halloween’ Burundi

Bujumbura, Burundi

MWANAMITINDO nyota nchini Burundi, Gurost Elmodo akishirikiana Ozine Moj wametikisa tasnia ya mitindo nchini humo kupitia tukio lao la Halloween.

Akizungumza na Mtanzania Digital kutokea nchini humo, Gurost amesema mapokezi yamekuwa makubwa licha ya wengi kudhani sherehe hizo ambazo hufanyika kila inapofika Oktoba 31, kila mwaka ulimwenguni kote zina uhusiano na ushirikina.

Katika hali ya kiwatuliza wapenzi wa ‘fashion’ nchini Burundi, Gurost na rafiki yake Ozine, wamesema lengo la kufanya Halloween Burundi ni kuchangamsha tasnia hiyo na si vinginevyo.

“Tulifanya Halloween hapa Burundi ili wanamitindo mbalimbali waonyeshe uwezo wao wa kutoka kitofauti na hakuna mambo ya ushetani kama wanavyosema wengine, nafurahi Halloween hapa Burundi imepokewa vizuri,” amesema Gurost.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles