25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Galawa ataka Halmashauri Songwe zibuni biashara mpya

chiku-galawaNa Eliud Ngondo, Songwe

MKUU wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa, ameziagiza halmashauri za wilaya mkoani humo kubuni biashara ambayo itakuwa na tija kwa kuongeza mapato bila kutegemea ushuru wa mazao.

Akizungumza jana Mjini Vwawa, Galawa alisema halmashauri zikiwa na miradi ya biashara zitakusanya fedha za kutosha na kuachana na ukusanyaji wa ushuru wa mazao ambao wananchi wamekuwa wakiulalamikia.

Alisema ubunifu wa biashara hizo utafungua fursa kwa vijana wasio na ajira na kuajiriwa kupitia miradi hiyo,  kufunguliwa kwa viwanda ambavyo vikisimamiwa na kufanyakazi kwa uhakika vitakuwa ni chanzo cha mapato.

“Mkoa wetu huu ni mchanga lakini inatakiwa tukazane kwa namna yoyote ile ili tuwe kama mikoa mikongwe, hivyo lazima kila halmashauri ijikite kubuni biashara ambayo itakuwa fursa kwa vijana kuongeza kipato,” alisema Galawa.

Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo walisema kubuniwa biashara kutafungua njia za kuongeza mapato.

Valery Kwembe ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mji wa Tunduma, alisema agizo hilo la mkuu wa mkoa linalenga kuinua mapato kuliko kuendelea kutegemea mapato kutoka katika vyanzo vya ushuru wa mazao pekee.

Vyanzo vya ushuru wa mazao vina msimu wakati mwingine mazao hakuna kabisa, sasa biashara zikifunguliwa itakuwa ni njia mojawapo ya kuzuia pengo hilo.

“Suala la kubuni biashara kwa kila wilaya mkoani Songwe litakuwa ni njia ya kukusanya mapato na kuacha kutegemea vyanzo ambavyo ni vya msimu pekee, lakini pia utegemezi kwa Serikali kuu utakuwa umepungua,” alisema Kwembe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles