31.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 5, 2022

Contact us: [email protected]

Wakonta apata kifaa cha kumsaidia kuandika

wakontaNA GEORGE KAYALA

MWANDISHI wa ‘script’ anayetumia ulimi kuandikia, Wakonta Kapunda, amepata kifaa cha kumsaidia kuandika kwa kutumia sauti ambacho ndiyo ameanza kukifanyia mazoezi.

Wakonta aliliambia MTANZANIA kwamba kupatikana kwa chombo hicho kiitwacho Nuance Dragon Naturally Speaking, kitamrahisishia kuandika kwa haraka script za filamu zake na mambo mbalimbali ambayo atataka kuyafanya.

“Kupatikana kwa kifaa hicho ni faraja kwangu kwasababu ninachotaka kukiandika nazungumza kupitia kipaza sauti chake kisha chenyewe kinaandika katika kompyuta,” alisema Wakonta huku akifurahia kifaa hicho.

Kifaa hicho kimetolewa na msamaria mwema, Olivia Soko ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Whirl Market Technologies kutoka Afrika Kusini aliyeguswa na hali ya mwandishi huyo kutokana na ajali aliyopata siku ya mahafali yake ya kidato cha sita miaka minne iliyopita na kumsababisha kupooza kuanzia shingoni kushuka chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,586FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles