24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

G7 WAKUTANA KUIJADILI URUSI

TORONTO, CANADA


MAWAZIRI wa Mambo ya Nje wa nchi saba zenye ushawishi mkubwa wa kiuchumi duniani (G7), wamekutana mjini hapa wakitafuta mwelekeo mmoja wa kuchukua dhidi ya Urusi.

Lakini kulingana na ofisa mmoja wa Marekani, mawaziri hao wameacha mlango wazi kwa majadiliano na Urusi.

Mataifa hayo yanahofia kile wanachokiona kama vitendo vya uchokozi wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin.

Miongoni mwa vitendo hivyo ni kumuunga mkono Rais Bashar al Assad na utawala wake nchini Syria, ambako vita vya wenyewe kwa wenyewe vinaendelea, kuimega Crimea kutoka Ukraine na madai ya jaribio la kumuua jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, alisema nchi za Magharibi ni lazima zishirikiane kusitisha hatua ya Putin ya kukandamiza demokrasia, ikiwamo usambazaji wa habari za uongo.

Mawaziri hao walitarajiwa kutoa taarifa ya mwisho kuhusu mkutano wao huo baadae jana.

Ofisa mmoja anayehudhuria mkutano huo, alisema mawaziri hao hawatatumia lugha nyepesi watakapotoa taarifa kuhusu Urusi kwa kuzingatia yaliyofanywa na nchi hiyo kufikia sasa.

Lakini kwa mujibu wa wanadiplomasia wawili katika mkutano huo, mawaziri hao hawatatangaza hatua kamili watakazoichukulia Urusi kutokana na sababu za kisheria.

Sababu hizo zinatokana na ukweli kwamba miongoni mwa mataifa hayo saba, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na Italia ni wanachama wa Umoja wa Ulaya, chombo cha mataifa 28, ambacho sharti kije na kauli moja kuhusu hatua za kuchukuliwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas, ameitaka Urusi kusaidia katika kusuluhisha mzozo wa Syria, akisema suluhu haiwezi kupatikana bila Urusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles