22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

MSHAMBULIAJI ALIYE NUSU UCHI AUA MAREKANI

TENNESSEE, MAREKANI


MTU aliyekuwa nusu uchi, amewaua watu wanne katika mgahawa mmoja huko Nashville katika jimbo la Tennessee nchini hapa.

Alianza kuwamiminia risasi watu waliokuwa katika mgahawa akiua watu wanne na kujeruhi wengine wawili.

Polisi wanaendelea kumsaka mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Travis Reinking mwenye umri wa miaka 29, mkazi wa Illinois.

Taarifa zinasema mwaka jana, Travis alishikiliwa na polisi pale alipojaribu kuingia katika eneo ambalo lipo karibu na Ikulu ya Marekani.

Hata hivyo, mmoja wa wateja mgahawani, James Shaw, alipongezwa kwa ujasiri aliouonyesha baada ya kumnyang’anya bunduki mshambuliaji huyo, ambaye huenda bila hatua hiyo angeua watu wengi zaidi.

Lakini James mwenyewe amekataa kuitwa shujaa akisema alikuwa akijaribu kujiokoa na kwamba si shujaa.

Sheria ya umiliki silaha nchini Marekani bado inatoa mwanya wa kuzagaa kwa silaha, hali ambayo inasababisha mashambulizi ya mara kwa mara ya silaha zinazomilikiwa na watu kirahisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,305FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles