28.8 C
Dar es Salaam
Monday, June 17, 2024

Contact us: [email protected]

FDH yatoa mafunzo ya lugha ya alama kwa watumishi wa Suma JKT

Na Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

KUTOKANA na changamoto ya mawasiliano iliyopo kwa watu wenye ulemavu hususan wasio sikia na wasioona katika taasisi mbalimbali zikiwemo za umma Shirika la kuhudumia watu wenye ulemavu (FDH) limetoa mafunzo ya lugha ya alama kwa watumishi wa Shirika la Uzalishaji mali la Suma JKT.

Mafunzo hayo yatasaidia watumishi wa shirika hilo kutoa huduma kwa makundi yote ikiwemo watu wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi) na wasioona.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Suma JKT, Luteni Kanali Dora Kawawa, amesema mafunzo hayo kwao ni fursa kubwa kwakuwa kupitia kampuni zao wanafanya kazi na watu tofati wakiwemo wenye ulemavu wa kutosikia.

“Nyinyi mnaoanza kupokea mafunzo haya ni wawakilishi katika shirika najua shirika linaandaa utaratibu na mafunzo haya yatakwenda kusambaa katika kanda zote kadri itakavyopangwa naomba tuchulie hii kama fursa ya kujua lugha ambayo itatusaidia kuwasiliana na kundi hili maalum ambalo ni miongoni mwa wateja wetu hivyo tutaweza kuwafikia,” amesema.

Luteni Kanali Kawawa amesema mafunzo hayo yatahusisha jinsi ya kuwasiliana kwa alama na namna ya kuwatambua watu wenye ulemavu wa kutosikia ili kujua nini wanataka na namna ya kuwahudumia.

“Kampuni yetu inafanya biashara na watu tofauti hivyo hatuna ubaguzi na lengo letu ni kuwafikia wateja wa aina zote,” amesema.

Aidha, amesema mafunzo hayo ya mwezi mmoja yatatolewa kwa wafanyakazi waliopo jijini Dar es Saalam na baada ya hapo wahusika watafanya kazi katika mkoa huo na mkoa wa Pwani.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa FDH, Maiko Salali, amesema kundi la watu wenye ulemavu ni miongoni mwa makundi yenye changamoto nyingi katika jamii ikiwemo kushindwa kuzifikia huduma muhimu kutokana na kukosa mawasiliano na watoa huduma hasa viziwi na wasioona.

“Mafunzo haya umuhimu wake ni kuwa yataongeza wigo wa mawasiliano baina ya watu wenye ulemavu hususani wasiosikia na wasaioona na watoa huduma katika utoaji wa huduma kwenye maeneo mbalimbali nchini,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles