24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Array

FCC yawanoa wahariri, yaitisha nyaraka mkataba wa GSM,TFF

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

TUME ya Ushindani Tanzania(FCC), imesema imetoa siku 21 kwa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwasilisha taarifa muhimu za mkataba wa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, GSM na tayari shirikisho hilo limeanza kupeleka nyaraka hizo kutokana na malalamiko ya wadau wa soka nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana Desemba 20, 2021 na Mkurugenzi wa FCC, William Erio wakati akifungua semina ya Wahariri wa Habari za Biashara iliyoandaliwa na tume hiyo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Suala la mkataba wa GSM linashughulikiwa sitaki kulizungumzia sana kwa sasa kwa sababu tumewapa TFF siku 21 kuleta taarifa muhimu na tayari zimeanza kuja,” amesema Erio.

Sababu ya FCC kuwanoa wahariri

Erio amesema lengo la FCC kuwapa semina wahariri wa habari za biashara ni kutaka kuwawezesha kuelimisha umma ambao ni walaji kuepuka bidhaa bandia na wafanyabiashara wafuate sheria na kuvutia watu wapya kuwekeza Tanzania.

“Kwa kutambua umuhimu na nafasi yenu katika vyombo vya habari kama wahariri na waandishi waandamizi wa habari za biashara,sisi FCC ndiyo shughuli yetu kubwa hiyo. Tumeona ni vema kuwajengea uwezo na kuwaongezea uelewa wenu, tunafikiri baada ya kumaliza tutakuwa tumefanikiwa,”

“Kimsingi shughuli zetu ni mbili, kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara hapa nchini. Kuhakikisha kila kinachofanywa hakikiuki sheria ya ushindani, pia tuna jukumu kubwa la kumlinda mlaji,” amefafanua Erio.

Baadhi ya Wahariri wa Habari za Biashara kutoka Vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mafunzo yaliyoandaliwa na FCC jana.

Kwa upande wake Katibu wa Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)Neville Meena, ameishukuru FCC kwa semina hiyo na kuwataka kuendelea kutoa nafasi hiyo kwa wanahabari ili wananchi waweze kuifahamu vizuri na shughuli zake.

“Nina ombi kwa ajili ya wanahabari wa ‘sports’, baada ya kundi hili kufikiria kukutana na waandishi wa sports kwa kuwa sasa hivi kuna uwekezaji mwingi wa kibiashara katika michezo,” amesema.

Yaeleza ukubwa wa tatizo la bidhaa bandia

Akitoa mada katika semina hiyo, Mkuu wa Idara ya Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Bidhaa Bandia, Magdalena Utouch, amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya kukabiliana na vitu bandia hasa kutokana na ukuaji wa teknolojia.

Magdalena ameeleza kuwa changamoto hiyo inachangiwa na uingizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na kukosekana kwa ofisi za Kanda ambapo wanatarajia kuzifungua.

Mkurugenzi wa FCC, William Erio akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Habari za Biashara na viongozi wengine wa FCC jana.

“Maana ya bidhaa bandia (feki)ni bidhaa zilizotengenezwa kwa kuiga bidhaa nyingine kwa nia ya kudanganya mlaji na mara nyingi huwa bidhaa duni na zina madhara makubwa kwa mlaji,” amefafanua.

Majukumu ya FCC

Kati ya majukumu ya FCC ni kuhakikisha hakuna makubaliano ya makampuni yaliyo kinyume cha FCA, kuchunguza na kuchukua hatua za kisheria kwa makampuni au mtu anayetumia vibaya nguvu ya soko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles