24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yatoa vifaa vya masomo kwa shule ya Sekondari Bonyokwa

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkonononi ya Halotel hapa nchini, imetoa vifaa mbalimbali kwa waalimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Bonyokwa ili kupunguza changamoto za mahitaji ya vifaa vya elimu zinazowakabili.

Akitoa taarifa hiyo leo Jumanne Desemba 21, wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kwa sababu ya kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo.

“Mpango huu ni kufungia Juhudi za Serikali ambaye zimekuwa katika kuhakikisha shule zote zinapata mahitaji mhimu ili kuwafanya wanadunzi kupata elimu katika mazingira bora,” amesema Makabu.

Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na meza na vitu vya waalimu, kabati la vitabu na mafaili, desktop mbili na printer ikiwa ni moja ya njia ya kurahisha ufundishaji na ufanisi katika masomo.

Pamoja na hayo Halotel inatoa huduma ijulikanayo kama “Halotstudy” itakayowawezesha wanafunzi nchini kusoma masomo yao kwa njia ya mtandao inayopatikana kwa simu ya mkononi na Kompyuta ambayo huduma hiyo ni bure ambapo kitakachotakiwa ni kuwa na huduma ya internet.

Kwa upande wa Mkuu wa shule ya Sekondari ya Bonyokwa, Upendo William, amesema kuwa ni faraja kwa kupokea msaada huu kutoka Kampuni hiyo.

“Tunaishukuru sana kampuni ya Halotel kwa kuendelea kuwa karibu na jamii na kuthamini jitihada na kuisaidia sekta ya elimu nchini,Kwani vifaa hivi vitawasiadia waalimu na wanafunzi katika masomo yao,” amesema Upendo.

Kwa Upande wa Diwani wa kata ya Bonyokwa, Tumila Malilo, mbali na kuishukuru Kampuni hiyo, amewaomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia katika sekta ya elimu.

“Tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kama ambavyo kampuni ya Halotel inavyohakikisha shule zinapata huduma kama hivi,” amesema Malilo.

Kwa upande wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Veronica Simbwe, ameishukuru Kampuni hiyo kwa kuwarahisishia upatikanaji wa masomo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles