27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yasaini makubaliano ya ulipaji wa Sh Trilioni 2.17 kwa watumishi wa Umma

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

WIZARA ya Fedha na Mipango imesaini mkataba wa makubaliano wa ulipaji wa Sh Trilioni 2.17 kwenda Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Emmanuel Tutuba, akidai Serikali imeona ni sahihi kupitia na kufanya malipo hayo kwa nia njema ya kuhakikisha sekta hiyo muhimu inaendelea kuhudumia Watanzania.

Akizungumza leo Desemba 22,2021 wakati wa hafla za utiaji saini wa makubalino ya ulipaji wa shilingi trilioni 2.17 kutoka Serikalini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba amesema wamekuwa na majadiliano ya mara kadhaa na PSSSF juu ya kushughulikia suala la deni la Pre 1999.

Amesema baada ya kufanya uchambuzi wa kina juu ya suala hilo na kwa maslahi mapana ya wanachama wa Mfuko huo serikali imeamua kulipa deni hilo kwa kuanzia na Sh trilioni 2.17 ambapo amedai deni hilo litalipwa kwa utaratibu wa hati fungani maalum ya miaka kuanzia 8 hadi 25.

“Serikali imeona ni sahihi kupitia na kufanya malipo hayo kwa nia njema ya kuhakikisha sekta hii muhimu inaendelea kuhudumia Watanzania na kushiriki vyema kwenye ujenzi wa uchumi wetu,” amesema.

Amesema takwimu za sasa PSSSF kila mwezi inalipa kiasi cha takribani Sh bilioni 60 kama pensheni kwa wastaafu kila mwezi ambapo amedai tafsiri yake kwenye uchumi ni kwamba kila mwezi PSSSF inatoa fursa ya Sh bilioni 60 kwenye uchumi.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma (PSSSF) CPA  Hosea Kashimba amesema kupitia mkataba huo wenye thamani ya Sh trilioni 4.66 ambao kwa kuanzia utaruhusu serikali kutoa hati fungani zisizo taslim (Non Cash Bond) za thamani ya shilingi trilioni 2.17 kwa muda wa kuanzia miaka 8 hadi 25.

Amesema uwekezaji huo utasaidia mfuko kupata mapato yanayotokana na hati fungani takribani Sh bilioni 120 kwa mwaka.

“Sisi kama PSSSF tunaamini kwamba utekelezaji wa jambo hili utawezesha Mfuko kupata unafuu wa deni la pre 1999  na pia kuuwezesha kutimiza jukumu lake la msingi la kulipa mafao.

Mkurugenzi huyo ameihakikishia serikali kila kiasi cha fedha kitakachopatikana kitaelekezwa kwenye maeneo kusudiwa ikiwemo uwekezaji ili kuongeza thamani na ukwasi wa mfuko na jukumu kuu la ulipaji wa mafao kwa wakati pindi wanachama wanapostahili kulipwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles