28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Familia ya aliyeuawa na polisi kulipwa bil. 34/-

COLORADO, Marekani

MAMLAKA za Jiji la Colorado zimethibitisha kuwa familia ya kijana aliyefariki baada ya kuchomwa sindano ya sumu na polisi italipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 15 (zaidi ya Sh bil. 34 za Tanzania).

Elijah McClain mwenye umri wa miaka 23,  alifariki mwaka 2019 mjini Aurora, ikiwa ni siku tatu tangu aliposimamishwa na polisi watatu na kisha kuchomwa sumu hiyo.

Familia yake ilifungua kesi kuwashitaki wanausalama hao na hii inakuwa ni fidia kubwa zaidi kuwahi kulipwa familia ya marehemu ndani ya Colorado.

Kwa upande wake, mama mzazi wa McClain, Sheneen, amewashukuru waliomuunga mkono katika kesi hiyo, pia akisema kifo cha mwanawe huyo kitaleta mapinduzi makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles