26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Faidika yazindua bidhaa mpya ya mikopo

EXEC PIX 1Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya kifedha, Faidika imezindua bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive’ inayolenga kuwezesha upatikanaji rahisi wa mkopo usiokuwa na dhamana kwa wafanyakazi wa serikalini wa mpaka Sh milioni 30.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Marion Moore, alisema mkopo huo mpya ni moja kati ya bidhaa ya kipekee nchini yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyakazi kutoka serikalini.
“Bidhaa yetu ya mkopo wa Executive, ni bidhaa itolewayo haraka yenye ubunifu na rahisi katika upatikanaji wake na ya kipekee katika soko la Tanzania.
“Ni mkopo ambao utawawezesha wafanyakazi wengi kutoka serikalini kupata fedha na kuweza kuinua viwango vyao vya maisha kwa kujihusisha na miradi mikubwa mbalimbali. Viwango vya mikopo hii ni kuanzia shilingi milioni 10 mpaka thelathini ambapo marejesho yake yanaanzia miezi sita mpaka sitini,” alisema Moore.
Naye Meneja Masoko wa Kanda wa Faidika, Haule Stephen, alisema mwombaji anatakiwa kutoa stakabadhi mbili za mishahara ya miezi miwili iliyopita, taarifa ya kibenki ya akaunti kuanzia miezi miwili na kuendelea, kitambulisho cha kazi na picha moja ya pasipoti ili kujipatia mkopo huo.
“Dhumuni letu ni kuona viwango vya maisha vya Watanzania vinakua kupitia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha,” alisema Stephen.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles