33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Exim Bank yapania kutoa misaada zaidi kwa jamii kwa mwaka 2017

Exim Bank imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatoa misaada mbalimbali kuihudumia jamii inayoizunguka. Misaada inayotolewa na benki hii kongwe ni ishara ya uzalendo na moja ya njia za kuishukuru na kuirudishia jamii sehemu ya mafanikio ya benki hiyo.

Sio jambo la kustaajabisha kuona taasisi hiyo ya kifedha ambayo imeanzishwa miaka 20 iliyopita kwa mtaji wa TZS Bilioni 12 na hadi kufikia mtaji wa TZS Bilioni 200 ikijumuika na jamii iliyoizunguka katika kusherekea mafanikio hayo. Pia ikitumia fursa hiyo kusema asante kwa wanajamii ambao ni ukweli usiopingika kuwa mchango wao wa hali na mali ndio umeifikisha benki hapo ilipo.

Mariam Mwapinga ni meneja masoko wa Exim Bank, “Kuna msemo usemao kuwa muhimili wa nchi yoyote ile ni wananchi ambao wapo tayari kujitolea kwa ajili ya jamii yao kwa namna moja au nyingine ili nchi yao ifikie malengo yake iliyojiwekea.”

[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=jmzSycuPciQ[/embedyt]

Hapa nchini,  hiki ndicho Exim Bank imekuwa ikifanya katika kuhakikisha kuwa jamii inafikia malengo yake iliyojiwekea. “Hapa Exim Bank kuna kitengo maalum ambacho kipo kwa ajili ya kusaidia jamii iliyotuzunguka kama kutoka shukrani na asante kwa kutufikisha hapa tulipo sasa”

Mariam anaendelea kutoa mifano kadhaa ambayo Benki ya Exim imeweza kutoa misaada kwa jamii kama ifuatavyo.

“Mifano michache ambayo Exim Bank imeweza kutoa katika kusaidia jamii ni moja ikiwepo maafa yaliyotokea Kagera.Ya pili ni kujitolea kwa madawati katika mikoa tofauti tofauti, kufanikisha zoezi la utoaji damu na kusambaza katika hospitali tofauti tofauti na jingine la mwisho ni kusaidia bustani mbalimbali zilizopo hapa jijini Dar es Salaam kuliboresha jiji letu na kuonekana la kuvutia”.

Sambamba na misaada hiyo ambayo Exim Bank imeitoa kwa jamii, benki hiyo imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa inaendelea kutoa misaada kwa jamii na kuwahakikishia watanzania wote kuwa mwaka huu wa 2017 wataendelea kufanya hivyo na kuiwezesha Tanzania kufikia malengo iliyojiwekea katika mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles