ABU DHABI, UAE
SHIRIKA la Anga la Etihad (EAG) limetangaza uteuzi wa Gavin Halliday kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hala Group lenye jukumu la kuboresha utendaji na huduma zake duniani.
Halliday ataliongoza shirika hilo kuendana na huduma bora duniani na kuwasogeza karibu wateja kuendelea kufurahia huduma zinazotolewa na shirika hilo na washirika wake wa ndege.
Pia atawajibika kuwa karibu na wabia wa EAG na kushiriki vikao vya utawala vilivyo muhimu kwa mipango na maendeleo ya ukuaji wa biashara baina ya Abu Dhab na nchi za Falme za Kiarabu (UAE).
Halliday anajiunga EAG baada ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu mkubwa wa miaka 30 katika Shirika la Ndege la Etihad na Kundi la Mashirika ya Kimataifa ya Ndege (IAG).