25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

ENGLAND YAFUNGA USAJILI KWA REKODI MPYA

LONDON, England

LIGI Kuu England usiku wa Oktoba 31, mwaka huu, ilifunga dirisha la usajili, huku klabu zikiwa zimevunja rekodi ya msimu uliopita ya pauni milioni 155 kwa kutumia jumla pauni milioni 210 katika siku ya mwisho ya usajili.

Licha ya klabu hizo kutumia jumla ya pauni bilioni 1.4 katika usajili wa dirisha hilo, baadhi ya wachezaji kama Alexis Sanchez, Virgil van Dijk, Riyad Mahrez, Thomas Lemar, Diego Costa na Ross Barkley waliendelea kubaki kwenye klabu zao.

Matumizi hayo ya fedha ni makubwa, yakilinganishwa na msimu uliopita ambapo ilikuwa pauni bilioni 1.1, huku ikiwa tofauti ya pauni bilioni 1 kwa usajili uliofanyika katika miaka mitano iliyopita kwa kila klabu kusajili katika uwiano wa pauni milioni 71, lakini mwaka 2016 ulikuwa uwiano wa pauni milioni 58.

Klabu ya Chelsea dakika za mwisho ilitumia pauni milioni 35 kumsajili Danny Drinkwater na Mamadou Sakho  kwa dau la pauni milioni 26 kutoka  Crystal Palace.

Klabu hiyo pia ilimsajili Davide Zappacosta, wakati Tottenham ikimsajili mshambuliaji wa Swansea, Fernando Llorente kwa uhamisho wa pauni milioni 15.

Lakini Swansea nayo iliziba nafasi hiyo kwa kumsajili Wilfried Bony kutoka Manchester City kwa pauni milioni 12.

Wakati huo klabu ya Liverpool ikiendelea kupiga chini ofa ya pauni milioni 114 kutoka kwa Barcelona waliokuwa wakivizia saini ya kiungo wao Philippe Coutinho, hata hivyo, nyota huyo milango ipo wazi kuhamia klabu hiyo kama watafikia makubaliano.

Mahrez na Costa pia walihusishwa kuondoka katika klabu zao na kutimkia Hispania, lakini bado kuna mazungumzo kati ya klabu zao zinazowahitaji na ikishindikana huenda wakasubiri hadi dirisha dogo la Januari, mwakani.

Ingawa Manchester City walishindwa kumsaijili Sanchez na beki wa West Brom, Jonny Evans, siku ya mwisho kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, ametumia pauni milioni 215 na kuifanya kuwa klabu pekee iliyotumia fedha nyingi katika usajili huo.

Hata hivyo, miongoni mwa klabu sita zilizotumia fedha nyingi katika usajili wa dirisha hilo ni pamoja na Paris St-Germain, iliyotumia pauni milioni 200 kumsajili Neymar dos Santos na Barcelona kumsajili Ousmane Dembele kwa pauni milioni 135 na kufanya wachezaji hao kuwa kati ya wachezaji  ghali wa muda wote.

PSG wao wameweka wazi dhamira yao ya kutumia pauni milioni 165 kumsajili  kinda wa Monaco, Kylian Mbappe mwaka 2018, baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo kwenye klabu hiyo.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles