23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Emirates yasifu mwelekeo wa uchumi Tanzania

LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM

MENEJA wa Kampuni ya Ndege ya Emirates Tanzania, Majid Al Falasi, amesema Tanzania itakuwa katika nafasi nzuri ya kiuchumi hapo baadae kutokana na wingi wa rasilimali na hatua zinazochukuliwa na Serikali kukuza uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Al Falasi alisema pia Tanzania ni moja ya nchini zenye soko iumara la usafiri wa anga kutokatana na wingi huo wa rasilimali na watu wanaosafiri kwenda sehemu mbalimbali za dunia.

Al Falasi alisema kitendo cha shirika hilo kutoa huduma kwa miaka 22 bila kuteteleka kunaonesha uwapo wa soko la uhakika na kwamba kutokana na kutoa huduma kwa kipindi kirefu wameweza kuyafahamu mahitaji ya Watanzania katika sekta hiyo.

“Uwapo wetu hapa Tanzania kwanza kunalenga kuboresha uhusiano wetu na Tanzania na kuiunganisha Tanzania na dunia. Tumeweza kusafirisha samaki, maua na nyama kwenda Ulaya na maeneo mengine ya dunia hii ni fursa nzuri kwa Tanzania na kwetu pia.

“Mazingira kutuwezesha kuwaunganisha Watanzania na dunia nzima huo kwetu ni uimara mkubwa wa soko la usafiri wa anga,” alisema Al Falasi.

Alidai kuwa hivi karibuni wanatarajia kuanzisha safari ya kutoka Dubai kwenda katika Jiji la Mexico kupitia Barcelona jambo ambalo litatoa fursa kwa wafanyabiashara wa kitanzania wanaosafiri kwenda huko kupata usafiri wa uhakika.

“Lakini pia tunaweza kumuunganisha haraka mfanyabiashara wa Tanzania na soko la London na Marekani na kuhakikisha hakosi chochote muda wote wa safari kwa sababu ndege zetu zote zimeunganishwa na internet anaweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida” alisema Al Falasi.

Wakati huo huo Al Falasi alisema kampuni hiyo inaungana na Serikali kupiga vita  matumizi ya vifungashio vya plastiki kwa kuviondoa kabisa katika safari zake zote na badala yake inatumia karatasi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles