WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Jeremy Hunt ameitaka Iran kuachia meli iliyokamatwa ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea.
Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Hunt ameitaka Iran kuichia meli hiyo kwa kile alichodaia imekamatwa kwa njia ya haramu.
Alisema meli hiyo, ilizingirwa na meli nne na helikopta kabla ya kuelekezwa eneo la maji la Iran.
Alisem “kuhusu usafiri majina lazima uimarishwe na hali itakuwa ” athari mbaya ” kama hali haitatatuliwa haraka..
” Hatuangalii hatua za kijeshi na kuongeza, tunatafuta njia za kidiplomasia za kutatua hali hii,”alisema
Jumamosi iliyopita, Hunt alituma ujume wa twitter uliosema: ” hatua ya jana katika eneo la Ghuba inaonyesha ishara za wasi wasi , Iran inaweza imechukua mkondo hatari wa kuyumbisha hali kinyume cha sheria, baada ya kumamatwa kwa meli ya mafuta katika eneo la Gibraltar kuelekea Syria.”
Shirika la habari linalomilikiwa na Iran (IRNA), limesema meli hiyo ilikamatwa baada ya kugongana na boti la uvuvi na kushindwa kujibu mawasiliano ya meli nyingine ndogo.
Taarifa zinasema, hakuna taarifa za majeruhi miongoni mwa wahudumu wa meli hiyo 23, ambao walikuwa uraia wa mataifa ya India, Urusi, Latvian na Ufilipino.
Msemaji wa serikali ya Uingereza, aliiiambia BBC kuwa : “Tumeshauri meli za mizigo za Uingereza kuwa mbali na eneo la Ghuba kwa muda .”Chombo cha kampuni ya Stena Impero ilikuwa ikisafiri majini ikiwa na bendera ya Uingereza na kusajiliwa London.
”Balozi wetu mjini Tehran anfanya mawasiliano na wizara ya mambo ya kigeni wa Iran kutatua hali hii na tunafanya kazi kwa karibu na washirika wetu wa kimataifa,” alisema.
Katika sauti zilizorekodiwa , meli ya Iran ilisikika ikiambia meli moja iliodaiwa kuwa Stena Impero -kubadilisha mkondo wake , ikisema kuwa iwapo utaheshimu utakuwa salama.
HMS Montrose inajitambulisha katika sauti hiyo iliopatikana na kampuni ya Uingereza kuhusu usalama wa majini Dryad Global.
Inaambia meli ya Stena Impero: wakati unaposafirisha mizigo katika mkondo wa bahari wa kimataifa na chini ya sheria za safari yako haifai kukatizwa ama kuzuiwa.